BUKOBA SPORTS

Friday, August 8, 2014

MKALI WA KOMBE LA DUNIA 2014, JAMES RODRIGUEZ APOKEA TUZO


Hatimaye James Rodriguez ametuzwa tuzo la mfungaji bora.

James Rodriguez akiwa na Tuzo zake

Rodriguez aliiwezesha Nchi yake kwenda Robo Fainali lakini walifungwa na  Brazil

Hatimaye mshambulzi wa Colombia James Rodriguez aliyeduwaza ulimwengu kwa kufunga mabao mengi zaidi katika kombe la dunia lililokamilika huko Brazil mwezi uliopita amepokea tuzo lake la mfungaji mabao mengi '' Golden Boot''.
Rodriguez ambaye aliyetikisa wavu mara 6 huko Brazil sasa anakibarua cha kutafuta namba huko Real Madrid dhidi ya wakinzani wenye haiba yake kama mchezaji bora msimu huu Christiano Ronaldo.


Rodriguez alinunuliwa na mabingwa hao wa kombe la mabingwa barani ulaya kutoka Monaco kwa pauni milioni 71.
Mshambulizi huyo mwenye umri wa miaka 23 alisema kuwa anamatumaini makubwa ya kutamba Santiago Bernabéu. 


Bao lake dhidi ya Uruguay katika robo fainali ya kombe la dunia limepigiwa upatu kutwaa tuzo la bao la mashindano japo Rodriguez mwenyewe anaikumbuka bao lake la kipekee dhidi ya Japan kuwa bora.
Colombia ilitegemea mabao yake sita katika mechi 5 kufuzu kwa hatua ya robo fainali kabla ya kuambulia kichapo cha 2-1 dhidi ya wenyeji Brazil.

No comments:

Post a Comment