Warnock, mwenye Miaka 65 na ambae alikuwa Palace kati ya Mwaka 2007 na 2010, amesaini Mkataba wa Miaka Miwili.
Mkongwe huyo mwenye makeke na vituko anachukuwa wadhifa kutoka kwa Tony Pulis ambae alibwaga manyanga Masaa 48 tu kabla Msimu mpya wa Ligi Kuu England kuanza hapo Agosti 16.
Msimu uliopita, Tony Pulis, aliteuliwa kuwa Meneja wa Msimu wa Ligi Kuu England baada ya kuiongoza Palace kutoka mkiani wakati akishika wadhifa huo kutoka kwa Ian Holloway Mwezi Novemba 2013 na kumaliza Ligi ikiwa Nafasi ya 11.
Warnock amekuwa hana kazi tangu Aprili 2013 alipoachana na Klabu ya Leeds United.
Mwaka 2010, Warnock aliondoka Palace baada ya Klabu hiyo kuwekwa chini ya Mwangalizi maalum ili kuepuka kufilisiwa, kitendo ambacho kiliifanya Klabu hiyo ikatwe Pointi 10 na kuiweka kwenye hali ngumu na nusura ishushwe kutoka Daraja la Championship.
Mwenyekti msaidizi Steve Parish alikuwa akitafuta Kocha mpya tangu Tony Pulis atimke zake Klabuni hapo.
Neil Warnock pia alishaiongoza Crystal Palacekati ya mwaka 2007-10, lakini pia alioongoza QPR
No comments:
Post a Comment