Hivi sasa Rojo yupo kwenye mgomo kufanya Mazoezi na Sporting Lisbon akishinikiza ahamie Man United na Klabu hiyo imesema itamwadhibu.
Mzozo huu umekuja baada ya Sporting Lisbon kuzuia Uhamisho wake wakitaka Dau kubwa kupita Ofa ya Pauni Milioni 16 waliyotoa Man United ili wao walipwe Fedha nyingi ingawa umiliki wao kwa Muargentina huyo ni Asilimia 25 tu.
Kampuni ya Doyen Sports, inayommiliki Rojo kwa Asilimia 75, imeijia juu Sporting Lisbon na kutishia kuchukua hatua za Kisheria ikiwa Klabu hiyo ya Ureno haitawalipa Asilimia 75 ya Ofa yeyote inayokataliwa.
Mkataba kati ya Doyen Sports na Sporting Lisbon unasema ikiwa mmoja kati yao atagomea kuuzwa Mchezaji huyo basi yule aliegoma anapaswa kumlipa mwingine Asilimia zilezile za umiliki wa Mchezaji huyo kulingana na Ofa iliyotolewa na kukataliwa.
Kwa sababu Sporting Lisbon ndio wanagoma kumuuza Rojo basi wao wanapaswa kuilipa Doyen Sports Pauni Milioni 12.
Rojo alihamia Sportung Lisbon Mwaka 2012 akitokea Spartak Moscow.
Sheria za Usajli Wachezaji England zinataka Mchezaji amilikiwe moja kwa moja na Klabu husika na ikiwa Man United watamtaka Rojo basi watapaswa kununua haki zake zote.
No comments:
Post a Comment