BUKOBA SPORTS

Monday, August 18, 2014

TIMU YA KAGERA SUGAR KUJIPIMA KWA KOMBAINI YA KAGASHEKI CUP JUMAMOSI HII AGOST 23.

Na Faustine Ruta, Bukoba
Timu ya KAGERA SUGAR itapambana na Timu Kombaini ya Kagasheki 2014 katika mchezo wa kirafiki utakaofanyika Jumamosi 23 Agosti 2014 kwenye Uwanja wa Kaitaba Bukoba Mjini
Mchezo huo wa kirafiki utakuwa maalumu kwa ajili ya kuwapima wachezaji waliosajiliwa katika timu hiyo kabla ya kuanza kwa Ligi Kuu ya Tanzania Bara. Na katika timu ya Kagasheki Kombani ni wale wachezaji waliomaliza katika Ligi ya Kagasheki mwaka huu 2014 kata 14 za hapa Bukoba na watajumuika kupata wachezaji watakaokipiga na Timu hiyo ya Kagera Sugar Inayocheza Ligi Kuu Tanzania Bara ya hapa Mkoani Kagera. Mchezo huo utachezwa  saa 10:00
jioni.Baadhi ya Wachezaji waliocheza Kagasheki 2014 Kata 14 hapa Bukoba wanatarajia kupambana katika Mchezo wa kirafiki Jumamosi hii kati yao na Kagera Sugar inayocheza Ligi Kuu Tanzania Bara kabla ya Msimu kuanza Sept. 20

Wachezaji Kombaini wakiwa na Kocha wao Kagire wakati wa mazoezi yao hivi karibuni wakijiweka sawa tayari kwa mchezo wa Kirafiki kati yao na Kagera Sugar.

Wachezaji Kombaini wa Kagasheki 2014

Baadhi ya Wachezaji wa Kagera Sugar wanaotarajia kupambana na Timu ya Kagasheki Kombaini jumamosi hii 23.08.2014  kujiandaa na Msimu mpya wa Ligi kuu Tanzania Bara 2014/15 inayotarajia kutimua Vumbi Sept. 20 mwaka huu.
Mtandao wa Bukobasports.com uliweza kuzungumza na mmoja wa waandaji wa Mtanange huo Bw. Mwinyi alisema anawaomba wapenzi wa soka wa Mkoa wa Kagera kuichukulia Timu ya Kagasheki Kombaini kuwa ni timu yao iliyotokana na Kata 14 zilishoshiriki Michuano ya Kagasheki mwaka huu 2014 kama ilivyo Kagera Sugar na waiunge mkono vilivyo kwani itacheza soka la kuwafurahisha na kukidhi kiu yao.

Kocha Msaidizi wa Kagera Sugar Murage Kabange(kushoto akiwa na Mwinyi wakiteta jambo kuhusu Mtanange huo wa jumamosi wiki hii katika Uwanja wa Kaitaba Bukoba Mjini.

No comments:

Post a Comment