BUKOBA SPORTS

Wednesday, August 27, 2014

UEFA CHAMPIONS LEAGUE: MARUDIANO - ARSENAL vs BESIKTAS, NANI KUIBUKA KIDEDEA!?

Arsenal leo wanatinga Uwanjani kwao Emirates kurudiana na Klabu ya Uturuki Besiktas kwenye Mechi ya Raundi ya Mwisho ya Mchujo ya UEFA CHAMPIONS LIGI.
Wiki iliyopita huko Instanbul, Besiktas na Arsenal zilitoka 0-0 na Arsenal wanahitaji ushindi tu ili kufuzu kwani Sare yeyote ya Magoli itamaanisha Besiktas ndio wataingia hatua ya Makundi ya UEFA CHAMPIONS LIGI ambayo Droo yake itafanyika huko Monaco Siku ya Alhamisi.
Arsenal wanaingia kwenye Mechi hii bila ya Kiungo wao mahiri Aaron Ramsey ambae alipewa Kadi Nyekundu kwenye Mechi ya Kwanza huko Instanbul.
Pia Arsenal itamkosa Nahodha wao Mikel Arteta mwenye tatizo la Enka na vile vile kumkosa Straika wao Olivier Giroud ambae pia ameumia Enka.
Kukosekana kwa Giroud kunaweza kutoa namba kwa Chipukizi Yaya Sanogo au Lukas Podolski au hata Alexis Sanchez kuchezeshwa kama Sentafowadi au ikibidi, Arsene Wenger kumtumia Joel Campbell.

Wakati Besiktas wana Kikosi kamili na Straika wao Demba Ba yu tayari kurejea tena Jijini London kuitesa Arsenal kama alivyokuwa akifanya akiwa na Klabu yake ya zamani Chelsea, Klabu hiyo ya Uturuki itakuwa bila ya Meneja wao kutoka Croatia kwenye Benchi, Slaven Bilić, ambae alipewa Kadi Nyekundu katika Mechi ya Kwanza na hivyo kulazimika kukaa Jukwaani kwa Mechi hii.Kocha wa Arsenal, Arsene Wenger

Bilic thinks Aaron Ramsey, centre, is Arsenal's best and most important player
Ba akishangilia na wenzake moja ya ushindi wao.
Demba Ba na wenzake wakipeta..
UEFA CHAMPIONS LEAGUE
RAUNDI YA MWISHO MCHUJO
Mechi zote kuanza Saa 3 Dakika 45 Usiku
Jumatano Agosti 27

Arsenal vs Besiktas (0-0)
Athletic Bilbao vs Napoli (1-1)
Bayer 04 Leverkusen vs FC Copenhagen (3-2)
Ludogorets Razgrad vs Steaua Bucharest (0-1)
Malmö FF vs FC Red Bull Salzburg (1-2)

No comments:

Post a Comment