City wanatarajiwa kumrejesha langoni Kipa wao Joe Hart baada ya Meneja Manuel Pellegrini kumpiga Benchi Mechi mbili Wiki iliyopita ile ya Capital One Cup walipoibamiza Sheffield Wednesday Bao 7-0 na Jumamosi kwenye Ligi walipoichapa Hull City 4-2.
Akikiri umuhimu wa Mechi hii, Pellegrini amesisitiza ushindi kwa Mechi yao hii ya Nyumbani lakini wana kibarua kigumu kwani AS Roma hivi sasa inawika na wako kileleni Serie A pamoja na Mabingwa Juventus baada wote kushinda Mechi zao 5 zote za mwanzo.
Pia, AS Roma huenda wakamchezesha Fulbeki wa zamani wa Chelsea, Ashley Cole, ambae sasa yuko na Klabu hiyo.
No comments:
Post a Comment