BUKOBA SPORTS

Wednesday, October 29, 2014

CAPITAL ONE CUP: MANCHESTER CITY 0 vs 2 NEWCASTLE, DOGO ROLANDO AARONS NA MOUSSA SISSIKO WAITOA KAMASI CITY ETIHAD!!

Moussa Sissoko alipowachambua mabeki wa City na Kuwachoma bao la pili na kuwapoteza zaidi City katika kipindi cha pili dakika ya 75 na kuwabwaga nje Man City amabo walikuwa Mabingwa Watetezi wa Capital One Cup.Ushindi huu wa Newcastle United unawafanya waendelee katika hatua inayofuata huku Mabingwa wa Ligi kuu England Manchester City safari yao inaishia hapo Etihad. Hapo hapo mchezaji wao matata David Silva aliumia mapema kipindi cha kwanza na kuondolewa baada ya kuumia mguu wake. Katika Mchezo mwingine Southampton wameifunga Stoke City bao 3-2. Spurs nao wameshinda bao 2-0.1-0, Newcastle United wanaongoza kwa bao lililofungwa mapema na Rolando Aarons dakika ya 6 Etihad. Bao la pili lilifungwa dakika ya 75 na Moussa Sissoko na kufanya 2-0 dhidi ya Man City na mbele ya Mashabiki 40,752. Newcastle sasa watacheza na Tottenham kwenye Robo Fainali.Dakika ya 6 kipindi cha kwanza Newcastle walipata bao la kuongoza kwa kufanya 1-0 Bao lililofungwa na Aarons baada ya kuwapita mabeki wa Man City.Jovetic kaanza.

No comments:

Post a Comment