BEKI wa QPR Rio Ferdinand amefungiwa Mechi 3 na kupigwa Faini ya Pauni 25,000 na FA, Chama cha Soka England, kutokana na Posti alizotoa kwenye Mtandao wa Twitter.
Ferdinand, mwenye Miaka 35 ambae ni Mchezaji wa zamani wa Manchester United na pia Nahodha wa zamani wa England, pia amepewa onyo kali kuhusu mwenendo wake wa baadae na vile vile kutakiwa kuhudhuria Programu ya Elimu ambayo itatayarishwa na FA.
Inaaminika Rio Ferdinand ameingia matatani baada kutumia neno "sket" kwenye Posti yake ya Twitter, neno ambalo ni lugha ya mtaani huko Jamaica ikimaanisha Msichana au Mwanamke malaya au Changudoa.
Kifungo hiki cha Mechi 3 kitamfanya Ferdinand azikose Mechi za QPR dhidi ya Chelsea, Man City na Newcastle.
Hata hivyo, katika Mechi mbili za QPR, Ferdinand amekuwa akiwekwa Benchi na Kocha wa QPR Harry Redknapp.
Posti hiyo ya Twitter iliyomtia mashakani Rio Ferdinand ilitolewa Septemba Mosi wakati akimjibu Mtu alieandika ‘Labda QPR itasaini Sentahafu mwingine kwa vile wanamhitaji’ na Rio kujibu: ‘Mwingize Mama yako, anacheza vizuri kiwanjani, mtoto! #sket’
Huko England, Rio Ferdinand anasifika sana kwa kuwa mchangiaji mzuri sana wa Mtandao wa Twitter akiwa ametoa Posti zaidi ya 14,000 tangu ajiunge Mwaka 2010.

No comments:
Post a Comment