MENEJA wa Manchester City Manuel Pellegrini amesema ana wasiwasi na fomu ya Timu yake kuelekea Dabi ya Jji la Mnchester itakayochezwa Jumapili Uwanjani Etihad.
Man City, Mabingwa Watetezi wa Capital One Cup, Jumatano Usiku walichapwa 2-0 Uwanjani kwao Etihad na Newcastle iliyokuwa na Kikosi cha Chipukizi wengi na kutupwa nje ya Mashindano hayo.
Kipigo hicho kinafuatia kile cha Wikiendi iliyopita walipofungwa 2-1 na West Ham kwenye Mechi ya Ligi Kuu England na kabla ya hapo waliumwaga uongozi wa Bao 2-0 na kutoka Sare ya 2-2 na CSKA Moscow kwenye Mechi ya Makundi ya UEFA CHAMPIONS LEAGUE.
Pellegrini ametoboa kuwa Wachezaji wake hawaaminiani na pia wanakosa imani na hivyo kutojiamini.
Kocha huyo kutoka Chile amesema: “Lazima tulikabili tatizo hili haraka. Tutajaribu kubadilika haraka.”
Kwenye Mechi ya Capital One Cup na Newcastle, Pellegrini alibadili Wachezaji 7 kutoka Kikosi kilichofungwa na West Ham na Kikosi hicho kuongozwa na Yaya Toure lakini pia kilikuwa na Wachezaji wa Kimataifa 10.
Jumapili City wanaikabili Man United iliyo chini ya Meneja Louis van Gaal ambayo haijafungwa katika Mechi 4 na wapo Nafasi ya 8 kwenye Ligi wakiwa Pointi 4 nyuma ya City walio Nafasi ya 3.
Akifafanua zaidi, Pellegrini alisema: “Nahisi hatuchezi vizuri. Tupo katika wakati mgumu na tunakosa kuaminiana. Tunafungwa Goli nyingi kirahisi na hatumalizii nafasi tunazopata.”
Pellgrini alikiri hali hiyo inawapa wasiwasi hasa baada ya kutoshinda katika Mechi zao 3 zilizopita ambazo walitoka Sare 1 na kufungwa 2.
Wakati huo huo, Pellegrini alikataa kuelezea undani wa kuumia kwa Wachezaji wake, Yaya Toure na David Silva, kwenye Mechi na Newcastle ambapo walilazimika kubadilishwa na pia alikataa kusema kama Wachezaji hao watakuwa fiti kuivaa Man United Jumapili.Yaya Toure

No comments:
Post a Comment