Kocha Mpya wa Coasta Union kutoka Nchini Kenya Yusuph Chippo akiwacheki Vijana wake kwenye Uwanja wa Kaitaba leo. Costal Union watacheza mchezo wao na Wenyeji Kagera Sugar kesho kwenye Mchezo wa Ligi kuu Vodacom. Jumla ya Wachezaji 18 wameongozana na Kocha huyo Raia wa Kenya Yusuph Chipo na Kesho Wanatarajia kukipiga na Wenyeji wao Kagera Sugar. Yusuph Chipo atakutana na Raia wa kigeni Mwenzake wa Uganda Jackson Mayanja ambaye ni Kocha wa Wakata Miwa Kagera Sugar. Picha na Faustine Ruta wa www.bukobasports.com
KOCHA wa timu ya Coastal Union ya Tanga, Yusuf Chipo akiteta jambo na Wachezaji wake leo kwenye Uwanja wa Kagera Sugar.
Kagera Sugar wako nafasi ya tano wakiwa na pointi 5 sawa na Mbeya City baada ya kutoka sare ya bila kufungana na timu ya Mjini Shinyanga Stand United, Huku Costal Union wakiwa nafasi ya 3 kwenye Msimamo wa Ligi kuu wakiwa na pointi 7.
Wachezaji wa Costal Union wakiwa makini kumsikiliza Mwalimu wao na kupanga mipango ya kutoka na Alama tatu muhimu kesho kwenye Uwanja wa Kaitaba. Picha na Faustine Ruta wa www.bukobasports.com
Wachezaji wa Costal wakijinyoosha Viungo
Kazi ipo kesho! nani kubuka kidedea Kaitaba.
Jumla ya Wachezaji 18 wamejifua leo kwenye Uwanja wa Kaitaba na hakuna majeruhi huku wengine wakitajwa kubaki jijini Tanga.
Wakati wa mapumziko kidogo
Kipa Shaaban Hassan Kado(wa pili kulia) wa Coastal Union nae aliambatana na kikosi
Wachezaji wa Costal union wakitoka Uwanjani baada ya Mazoezi yao kumalizika kwa siku ya leo Ijumaa kabla ya kukutana na Kagera Sugar kesho jumamosi Kaitaba
Baada ya Kumaliza Mazoezi
Wakiteta jambo!
Mchezaji wa Costal Union Razack Alphan
No comments:
Post a Comment