BUKOBA SPORTS

Friday, October 24, 2014

EUROPA LEAGUE: TOTTENHAM 5 vs 1 ASTERAS TRIPOLIS, HARRY KANE APIGA HAT-TRICK, EVERTON YABANWA! YATOKA SARE!

Harry Kane akishangilia..Bao tatu(Hat-Trick) za Harry Kane kwenye Mechi ya Kundi C la EUROPA LIGI limeipa Tottenham ushindi wa Bao 5-1 walipoitwanga Asteras Tripolis ya Ugiriki Uwanjani White Hart Lane.

Bao nyingine za Tottenham zilifungwa na Erika Lamela Mchezaji wa Argentina ambae alimalizia Mechi hii akiwa Kipa na kufungwa Penati baada ya Kipa Hugo Lloris kutolewa nje kwa Kadi Nyekundu iliyozaa Penati hiyo katika Dakika ya 87.
Everton, wakicheza Ugenini Mechi ya Kundi H, walitoka Sare 0-0 na Lille ya France.
Nao Celtic, wakicheza kwao Mechi ya Kundi D, waliifunga Astra Giurgiu, Bao 2-1.

KUNDI C
Partizan Belgrade 0 vs 4 Besiktas

Tottenham 5 vs 1Asteras Tripolis 


KUNDI H
FK Krasnodar 2 vs 4 VfL Wolfsburg
 Lille 0 vs 0 Everton



No comments:

Post a Comment