BUKOBA SPORTS

Thursday, October 23, 2014

KOCHA WA BARCELONA FC, LUIS ENRIQUE TUMBO JOTO! KUELEKEA MCHEZO WA "EL CLASICO" WA JUMAMOSI DHIDI YA REAL MADRID, ASEMA MATOKEO YOYOTE KWAO NI SAWA.


JUMAMOSI ndio Siku ambayo Vigogo wa Soka huko Spain, Real Madrid na FC Barcelona, watakapocheza Mechi yao ya kwanza ya La Liga Msimu huu Uwanjani Santiago Bernabeu kwenye pambano ambalo hubatizwa Jina rasmi ‘El Clasico.’
Safari hii, licha ya kuwapambanisha wale Masupastaa bora Duniani, Cristano Ronaldo, ambae ndiie rasmi Mchezaji Bora Duniani, na Lionel Messi, pia atakuwepo Mfungaji Bora Duniani, James Rodriguez, alietwaa Buti ya Dhahabu ya Fainali za Kombe la Dunia huko Brazil, akiichezea Real Madrid katika El Clasico yake ya kwanza.
Kivutio kingine, akicheza El Clasico yake ya kwanza, ni Straika mpya wa Barcelona, Luis Suarez, ambae hii huenda ikawa ni Mechi yake ya kwanza rasmi kuichezea Barca baada ya kumaliza Kifungo chake cha Miezi Minne alichopewa huko Brazil Mwezi Juni baada ya kumng’ata Beki wa Italy, Giorgio Chellieni, kwenye Mechi ya Fainali za Kombe la Dunia.
Pia Barca watatinga kwenye Mechi hii wakiwa chini ya Meneja mpya, Luis Enrique, alietwaa wadhifa mwishoni mwa Msimu uliopita baada ya kutimuliwa Gerardo Martino ambae aliiongoza Barca kumaliza Msimu uliopita wakiwa kapa bila Kombe lolote.

Baada ya jana Barcelona FC kumtandika Eibar magoli 3-0 , kocha wa Barcelona, Luis Enrique amesema kwamba bado haamini kama matokeo hayo ni tafsiri sahihi ya kitakachotokea Jumamosi Oct 25, 2014 watakapo kutana na Real Madrid dimbani Estadio Santiago Bernabeu.

"Malengo yetu ni kuhakikisha tunapata alama tatu muhimu Jumamosi dhidi ya Real Madrid kwenye mchezo mzuri "El Clasico" utakao wakutanisha mahasimu wakubwa wa kandanda nchini Hispania, kumbuka endapo tukishinda maana yake ni kwamba tutazidi kujikita kileleni mwa ligi huku tukiwa tumemuacha mpinzani wetu mkubwa Real Madrid kwa jumla ya point saba.
"Lakini, kwa upande wangu bado naona matokeo ya aina yeyote katika mechi ya Jumamosi bado haitoa tafsiri halisi ya nani atakuwa bingwa wa Laliga kwa kuwa bado ligi ni mbichi kabisa, ila pamoja na hayo yote Wakatalunya sisi tunahitaji alama tatu muhimu Jumosi". Hiyo ndiyo kauli ya Luis Enrique jana baada ya mechidi ya Eibar.

Kumbuka katika hiyo mechi ya Jumaosi "El Clasico", ndiyo Barcelona wanatarajia kumtumia kwa mara ya kwanza mshambuaji wao LuisSuarez ambaye amekuwa nje ya dimba kwa muda wa miezi minne akitumia adhabu ya utovu wa nidhamu. FIFA ilimfungia Suarez kucheza mpira kwa miezi minne baada ya kumg'ata beki ya Italy Giorgio Chiellini wakati wa michuano ya kombe la mwaka huu nchini Brazil.

No comments:

Post a Comment