BUKOBA SPORTS

Thursday, October 23, 2014

LUIS VAN GAAL AMSOGEZA KIPA VICTOR VALDES OLD TRAFFORD BAADA YA KUWA HURU AKITOKEA BARCELONA.

KIPA wa zamani wa Barcelona Victor Valdes ameanza Mazoezi na Manchester United baada ya kuwa nje kwa muda mrefu akipona Goti lake aliloumia vibaya.Victor Valdes is a free agent after he did not renew his contract with Barcelona at the end of last season 
Valdes, mwenye Miaka 32, aliumia Goti hilo Mwezi Machi na kulikosa Kombe la Dunia kuichezea Nchi yake Spain.
Kabla ya kuumia, Valdes alikuwa ameshatoa uamuzi wa kuondoka Barcelona mwishoni mwa Msimu uliopita baada ya kukataa kuongeza Mkataba wake uliokuwa ukimalizika.
The Spanish goalkeeper lies on a stretcher after sustaining a serious knee injury in March of this year 
Inasemekana Meneja wa Man United, Louis van Gaal, ndie aliemkaribisha Valdes kufanya Mazoezi na Klabu yake wakati akiendelea kujiweka fiti baada ya kupona.
Former Barcelona goalkeeper Victor Valdes, pictured in 2011, is in talks with Manchester United over a move 
Taarifa kutoka Man United ilisema: “Valdes atakuwa chini ya uangalizi wa Madaktari wa Manchester United akiendelea kupona Goti lake wakati akisubiri kuanza Mazoezi na Timu ya Kwanza.”
Hata hivyo, Man United, ambae Kipa wake wa kwanza ni Mhispania David De Gea na Nambari mbili ni Anders Lindegaard, haijapasua kama itampa Mkataba Valdes.

No comments:

Post a Comment