Kikosi cha Kagera Sugar kilichoanza dhidi ya Stand United
Tayari kwa kipute kuanza...
kipute kimeanza...Mpira ulianza kwa kasi
Salum Kanoni akimlinda straika wa Stand United
Sehemu ya Viongozi wa Kagera Sugar na wachezaji wa Akiba
Kocha Mkuu wa Stand United(kulia) akiwa na Viongozi wengine pamoja na wachezaji wa akiba wakitazama mchezo wao na kagera Sugar huku ikiwa ni mara yao ya kwanza kufika Bukoba.
hapa hukatizi!!!
Kipindi cha kwanza kilimalizika vyema lakini kipindi cha pili kilikuwa ni shidaaa!! Kipa wa Kagera akikwaruzana na mchezaji wa Stand united katika kipindi cha pili dakika za mwishoni.
Patashika ilitokea...
Mwamuzi alisogea karibu kuwaachanisha!!
Tulieni!!! Poteza poteza Muda ikapita!
Aliyeumia tayari msaada wa haraka Uwanjani!
Akipelekwa nje ya Uwanja kuapata matibabu ya haraka
Muda unaenda kasi!! bado ni 0-0 Viongozi wa Kagera wakijiuliza hapa kunani!! mpaka sasa 0-0.
Kushoto ni Mwamuzi aliyechezesha kati Mchezo huu akitoka nje ya Uwanja baada ya dakika 90 kumalizika, Timu zote zikimalizika 0-0. Kagera walipata bao kipindi cha pili lakini bahati haikuwa yao Mwamuzi alidai kuna majanga yalitokea! Mchezaji kabla ya ufunga bao hilo aliunawa!
Dakika ya 90 zimemalizika!
G-Sengo kutoka Mwanza nae alikuwepo Uwanjani hapo kaitaba na hapa alikuwa akichukua habari kutoka kwa Kocha Mkuu wa Stand United Emmanuel Massawe baada ya mpira kumalizika!
Kocha wa Kagera Sugar Jackson Mayanja akihojiana na baadhi ya waandishi wa habari baada ya mpira kumalizika!
Mashabiki na wapenzi wa Stand United wakishangilia baada ya mira kumalizika kwa 0-0 kwenye Uwanja wa Kaitaba.
Na hapa Ngwasuma ilianza kuchukua kasi na nafasi!!
Yoote ni juu ya sare ya Ugenini!
No comments:
Post a Comment