BUKOBA SPORTS

Saturday, October 18, 2014

KLABU YA NEWCASTLE UNITED KUPIMA WACHEZAJI WAO WAAFRIKA EBOLA!

NEWCASTLE imeamua kuchukua hatua kujikinga na Ugonjwa wa Ebola kwa kuwapima Wachezaji wao wanaorejea Klabuni baada ya Mechi za Kimataifa toka Barani Afrika.
Gonjwa la Ebola limeikumba Afrika Magharibi na kuua Watu zaidi ya 4,000 na hivi sawa huko Uingereza Vituo vya Forodha vya Majini na kwenye Ndege Watu hupimwa Ugonjwa huo.
Newcastle midfielder Cheick Tiote has been playing in Africa Cup of Nations qualifiers for the Ivory Coast
Sasa Klabu ya Newcastle nayo imeamua kuwapima Wachezaji wao Waafrika wanaorejea Klabuni baada ya kucheza Mechi za Kimataifa na Nchi zao.
Wachezaji wa Newcastle, Papiss Cisse, anaetoka Senegal, na Cheik Tiote, wa Ivory Coast, walikwenda Nchini mwao na pia kusafiri na Timu zao kucheza Mechi za Makundi za AFCON 2015 huko Tunisia na Congo DR.

Meneja wa Newcastle, Alan Pardew, amekiri Klabu yao watakuwa wapuuzi ikiwa hawaukubali Ugonjwa huo.
Pardew ameongea: “Tunao mkakati wakirudi wao na Familia zao wataangaliwa. Hii ni kuwalinda na kuwasaidia.”
Nchi 3 tayari zilishapigwa marufuku na CAF kucheza Mechi kwao baada ya kuvamiwa na Ugonjwa huu na hizo ni Liberia, Guinea na Sierra Leone

No comments:

Post a Comment