MABINGWA Manchester City wakicheza kwao Etihad wameichapa Tottenham Bao 4-1 katika Mechi ya Ligi Kuu England na Bao zote kufungwa na Straika wao wa Argentina Sergio Aguero ambae pia alikosa Penati moja huku nao Spurs wakikosa Penati iliyopigwa na Roberto Soldado.
Mara baada ya Mechi, Meneja wa Man City, Manuel Pellegrini, amefananisha umuhimu wa Aguero kama ule wa Cristiano Ronaldo kwa Real Madrid na Lionel Messi kwa Barcelona.
Manchester City walifunga Bao lao la kwanza Dakika ya 13 baada ya Erik Lamela kuporwa Mpira Mita 30 toka Golini na Frank Lampard kumpasia Sergio Aguero alieachia Shuti na kutinga wavuni.
Dakika mbili baadae Tottenham wakasawazisha kufuatia Pasi ya Roberto Soldado kumkuta Christian Eriksen alieachia kigongo na kutinga.
Kwenye Dakika ya 19, Erik Lamela akamwangusha Lampard na Refa Jon Moss akatoa Penati iliyofungwa na Sergio Aguero.
City walimpoteza Lampard Dakika ya 26 baada kuumia Pajani na nafasi yake kuchukuliwa na Fernandinho.
Sentahafu wa Tottenham Younus Kabul alimwangusha David Silva katika Dakika ya 31 na Refa Jon Moss kuwapa Penati ya Pili City lakini Sergio aguero alikosa baada Kipa Hugo Lloris kuokoaa kwa Mguu na Mpira kumrudia tena Aguero aliepaisha.
Kipindi cha Pili, Aguero alifunga Bao la Tatu katika Dakika ya 68 kwa Penati iliyotolewa baada ya yeye mwenyewe kuvutwa Jezi na Federico Fazio alitolewa nje kwa Kadi Nyekundu.
Dakika ya 75, Aguero alipiga Bao lake la 4 na kuipa ushindi Man City wa Bao 4-1.
No comments:
Post a Comment