BUKOBA SPORTS

Saturday, October 25, 2014

KAGERA SUGAR 1 vs 1 COASTAL UNION, MAMBO MAGUMU TENA KAITABA!! SARE TENA LEO! SALUM KANONI APIGWA KADI NYEKUNDU! KOCHA JACKSON MAYANJA NAE AUTAZAMIA MPIRA NJE!

Kikosi cha timu ya Kagera Sugar kilianza kuumana na Kagera Sugar leo hii kwenye Uwanja wa KaitabaKikosi cha Costal UnionKagera walianza kipute hiki kwa kasi sana na kufanikiwa kupata bao kipindi cha kwanzaBenjamini Asukile akipanga kumtoka mchezaji wa Costal Union(kushoto).
Wachezaji wa Kagera wakishangilia bao lililofungwa na Paulo dakika ya 27 kipindi cha kwanza.Hata hivyo Kagera walibaki wachezaji 10 kipindi cha pili uwanjani baada ya mwenzao Salum Kanoni kuoneshwa kadi nyekundu.
Kipindi cha kwanza Kagera walipata bao kupitia kwa Paulo Maono aliyeingia kipindi cha kwanza na kufunga bao dakika ya 27.
Kipindi cha pili nao Coastal walisawazisha bao dakika ya 55 kupitia kwa Rama Salim aliyewatoka mabeki na kubaki na kipa wa Kagera Sugar na kumfunga.
Mpira huu haukumalizika vizuri kwani kipindi cha pili Salum Kanoni alioneshwa  kadi nyekundu na Mwamuzi katika dakika ya 60. Na pia kocha wao Jackson Mayanja alitolewa nje ya kikosi cha Ufundi baada ya kutoa malalamiko kwa mshika kibendera. Hivyo Kocha huyo kulazimika kuuangalizia mpira huu akiwa nje kama mashabiki wengine.
Salum Kanoni akitoka nje ya Uwanja akiwa kifua Wazi baada ya kutolewa kwa kadi nyekundu Kocha wa Kagera Sugar Jackson Mayanja akitolewa nje ya Uwanja na Mwamuzi What!!! Out!Kwa machungu Kocha wa Kagera Sugar Jackson Mayanja akitoka nje ya Uwanja!Hatari tupu leo!! Kocha Jackson Mayanja alimwachia kazi Kocha Msaidizi Kocha wa Kagera Sugar Jackson Mayanja  aliutazamia nje nusu ya mtanange wa leoLeo!!Kocha wa Costal Union Yusuph Chipo alibaki akishangaa huku akiutazama mpira kwa pande zote mbili.Dakika 90 zilimalizika kwa 1-1 timu zote mbili kwa kugawana pointi moja moja. Mtanange unaofuata kwa kagera wiki Ijayo ni Yanga.

No comments:

Post a Comment