Austin ndie aliyeifungia QPR bao zote mbili. Bao la kwanza lilifungwa na Charlie Austin katika kipindi cha kwanza dakika ya 17. Bao la pili lilifungwa tena nae kipindi cha pili dakika ya 69 na kufanya 2-0 dhidi ya Aston Villa kwenye Uwanja wa Loftus Road. Ushindi huu unawapandisha pointi moja kutoka mkiani mwa ligi na kupata pointi 7 na kuwaacha Burnley Mkiani wakiwa na pointi 4. QPR wakipanda hadi nafasi ya 19. Aston Villa pamoja na kufungwa bao 2-0 na QPR wamebaki nafasi ya 15 wakiwa na pointi 10.

Kocha wa QPR Harry Redknapp akiwa tayari Loftus Road kuangalia Vijana wake kama watautoa leo ili kujikwamua mkiani!

Rio Ferdinand nae kwenye benchi

Aston Villa walipo!
VIKOSI:
QPR: Green, Isla, Dunne, Caulker, Yun, Vargas, Henry, Sandro, Fer, Zamora, Austin.
Akiba: Traore, Hill, Phillips, Kranjcar, Murphy, Hoilett, Ferdinand.
Aston Villa: Guzan, Lowton, Vlaar, Clark, Cissokho, Cleverley, Westwood, Sanchez, Agbonlahor, Benteke, Weimann.
Akiba: Okore, Bacuna, Cole, Richardson, Bent, N'Zogbia, Given.
Refa: Lee Mason
No comments:
Post a Comment