BUKOBA SPORTS

Sunday, October 19, 2014

QPR 2 vs 3 LIVERPOOL, STEVEN CAULKER AIPA USHINDI LIVERPOOL! QPR WAENDELEA KUSOTA MKIANI!!!

Wachezaji wa Liverpool wakipongezana baada ya kuinyonga QPR kwao kwenye Ushindi wa mwishoni ambao unamajanga mengi yakiwemo kujifunga bao mbili QPR likiwemo la mwisho la kuwapa Ushindi Mtamu Liverpool. Ushindi huu unawapandisha Majogoo Liverpool nafasi ya tano huku QPR wakishikilia nafasi ya mwishoni ya 20 kwenye Ligi kuu hiyo ya England. Bao la kujifunga Queens Park Rangers kipindi cha pili dakika ya 67 na Richard Dunne limewaongoza Liverpool lakini bila ya kutegemewa QPR walisawazisha dakika ya 87 kupitia kwa Edu Vargas na kufanya 1-1. Baadae dakika ya 90 Coutinho alifunga bao la pili baada ya kufanya juhudi binafsi ndani ya box akilishwa mpira na Steven Gerrard. Ndani ya dakika nne(4) za nyongeza QPR walipiga kona kupitia kwa Leroy Fer na Edu Vargas kusawazisha bao kwa kufanya 2-2. Dakika za mwishoni za dakika ya 90 tena Steven Caulker alijifunga bao na kuwapa Ushindi wa pointi tatu Liverpool.Richard Dunne wa QPR akijifunga bao kipindi cha pili.
Ushindi wa Liverpool Unawapandisha mpaka nafasi ya tano huku QPR wakiendelea kusotea Mkiani wakiwa nafasi ya 20.Upande mmoja hoi!! kulia ni Majogoo Liverppool wakipongezana baada ya kushinda leo mwishoni kwenye dakika ya lala salama huku QPR wakijifunga bao hilo.

No comments:

Post a Comment