Akiongea kabla ya Jumatatu Usiku kwenda Ugenini huko The Hawthorns kucheza Mechi ya Ligi Kuu England dhidi ya West Bromwich Albion, Van Gaal amesema: “Hakuna Mtu atakaerudi kwenye Timu. Ni lazima ujitume Mazoezini na kila Mchezaji anajua hilo. Naheshimu Wachezaji wote ninaowatumia sasa na nawaamini Wachezaji hawa.”
Aliongeza: “Ukiwataja Rooney, Carrick na Jones ni Wachezaji wakubwa lakini tunao Wachezaji wengi wakubwa. Wakati mwingine Wachezaji wengine wanacheza vizuri zaidi. Mfano yule Chipukizi Paddy McNair alicheza vizuri mno katika Mechi yake ya kwanza na Mashabiki walimshangilia kila mara!”
Hata hivyo, Man United ililazimika kuwatumia Chipukizi wengi mwanzoni mwa Msimu baada ya kukumbwa na Majeruhi wengi lakini Juzi Van Gaal alitoboa kuwa hivi sasa Majeruni ni Wanne tu, ambao ni Mabeki Jonny Evans na Paddy McNair na Mawinga Jesse Lingard na Antonio Valencia lakini pia Man United itamkosa Nahodha Wayne Rooney ambae anatumikia Kifungo chake cha Mechi 3 kwa Kadi Nyekundu na Mechi na WBA itakuwa yake ya pili Kifungoni.
Hali hii imeleta matumaini kwa Mashabiki wa Man United ambao baada ya kuiona ikisuasua mwanzoni sasa imeonja ushindi katika Mechi mbili mfululizo dhidi ya West Ham na Everton lakini Van Gaal amesisitiza kuwa hali ya kusuasua si sababu ya kukosa Wachezaji tu.
Amefafanua: “Nimeshasema si Wachezaji wenye majina ndio bora. Nataka kila Mchezaji awe na bidii kiuchezaji hasa Mazoezini na kucheza Kitimu. Tukifanya hivyo Mazoezini, matokeo yatakuja tu, nina hakika na hilo!”
Lakini wapo wanaohoji kwanini Man United hawakuimarisha Difensi yao mwanzoni mwa Msimu na Van Gaal amefafanua kwa kusema: “Tuliwakosa Masentahafu Watatu walioumia. Hii ni kawaida kwa Klabu? Sidhani na baadae Jones na Valencia wakaumia sasa hao Mabeki Watano. Lakini kama tukinunua Mabeki Watano watachezaje hao wengine wakipona? Ndio maana nafanya kazi na Wachezaji 26 na si 35.”
No comments:
Post a Comment