West Ham United Leo hii wamewachapa Mabingwa Watetezi Manchester City Bao 2-1 katika Mechi ya Ligi Kuu England iliyochezwa Upton Park.
West Ham walifunga Bao lao la kwanza Dakika ya 22 baada ya pasi murua ya Alex Song kuipasua Difensi na kukumkuta Enner Valencia aliemsogezea Morgan Amalfitano ambae alimchambua Kipa Joe Hart stranded na kufunga.
Kipindi cha Pili Dakika ya 75 Diafra Sakho aliipa west Ham Bao la Pili lakini City wakafuga Bao lao pekee Dakika 2 baadae kupitia David Silva na kuleta wasiwasi mkubwa kwa Wenyeji.
No comments:
Post a Comment