JUMAPILI ipo Dabi ya Jiji la Manchester Uwanjani Etihad wakati Mabingwa Watetetezi Manchester City watakapoikaribisha Manchester United kwenye Mechi ya Ligi kuu England na kila Timu itaingia kwa kuwakosa Mastaa wao.
Wakati Man United wana habari njema za kurudi dimbani Nahodha wao Wayne Rooney aliekuwa amefungiwa Mechi 3, Man City watamkosa Mchezeshaji wao mahiri David Silva ambae ameumia na inasemekana atakuwa nje Mwezi mzima.
Pia Man City wana wasiwasi na kuwa fiti na Kiungo wao Yaya Toure ambae aliumia kwenye Mechi ya Jumatano Usiku wakati City inachapwa 2-0 na Newcastle na kubwagwa nje ya Capital One Cup Kombe ambalo wao walikuwa Mabingwa.
Meneja wa Man United Louis van Gaal alithibitisha kucheza kwa Rooney lakini pia alisema Radamel Falcao hatacheza kwani bado ana maumivu.

No comments:
Post a Comment