BUKOBA SPORTS

Saturday, November 29, 2014

LA LIGA: MALAGA 1 vs 2 REAL MADRID, MECHI 16 BILA KICHAPO!! REAL WASHEREKEA! WAPO KILELENI

BAO la kwanza la Real Madrid lilifungwa na Karim Benzema dakika ya 18 kipindi cha kwanza na mtanange kwenda mapumziko Real wakiwa mbee ya bao 1-0 dhidi ya Malaga.Kipindi cha pili Bale aliwafungia bao la pili na kufanya 2-0 baada ya kupokea mpira wa kichwa kutoka kwa Cristiano Ronaldo.
Bao la kwanza, Krosi ya Ronaldo ilimaliziwa vyema na Karim Benzema na kwa Bao la Pili Kichwa cha akili cha Ronaldo kilimfungulia njia Gareth Bale kupiga Bao la Pili.
Kipindi cha Pili Kiungo wa Real Isco alitolewa nje kwa Kadi Nyekundu baada ya kuzoa Kadi za Njano mbili.
Roque Santa Cruz ndie aliwafungia Malaga Bao la moja.
Rekodi ya kushinda Mechi 16 mfululizo chini ya Meneja Carlo Ancelotti imevunja ile ya Mechi 15 mfululizo iliyowekwa na Timu za Real za Mameneja Jose Mourinho Mwaka 2011 na Miguel Munoz Mwaka 1961.
Ushindi huu wa Real umewabakisha kileleni wakiwa Pointi 5 mbele ya Timu ya Pili Barcelona ambao Leo wako Ugenini kucheza na Valencia.

MECHI 16 WALIZOSHINDA REAL MDRID
1. Real Madrid 5-1 Basel (Champions League) - September 16
2. Deportivo la Coruna 2-8 Real (La Liga) - September 20
3. Real 5-1 Elche (LL) - September 23
4. Villarreal 0-2 Real (LL) - September 27
5. Ludogorets 1-2 Real (CL) - October 1
6. Real 5-0 Athletic Bilbao (LL) - October 5
7. Levante 0-5 Real (LL) - October 18
8. Liverpool 0-3 Real (CL) - October 22
9. Real 3-1 Barcelona (LL) - October 25
10.UD Cornella 1-4 Real (Copa del Rey) - October 29
11.Granada 0-4 Real (LL) - November 1
12. Real 1-0 Liverpool (CL) - November 4
13. Real 5-1 Rayo Vallecano (LL) - November 8
14. Eibar 0-4 Real (LL) - November 22
15. Basel 0-1 Real (CL) - November 26
16. Malaga 1-2 Real (LL) - November 29

No comments:

Post a Comment