Mabingwa Watetezi wa Ligi Kuu England Manchester City wameichapa Southampton Bao 3-0 na kuishusha toka Nafasi ya Pili na wao kuikamata sasa wakiwa Pointi 6 nyuma ya Vinara Chelsea.
Yaya Toure aliipa Man City Bao la Kwanza katika Dakika ya 51 lakini wakapata balaa katika Dakika ya 74 baada Sentahafu wao Eliaquim Mangala kutolewa kwa Kadi Nyekundu baada Kadi za Njano mbili.
Licha ya kuwa pungufu, Frank Lampard aliifungua Man City Bao la Pili katika Dakika ya 80 baada ya kupokea pasi James Milner.
Gael Clichy alifunga Bao la 3 katika Dakika ya 88 baada ya pasi murua ya Sergio Aguero.
No comments:
Post a Comment