Kevin Mirallas wa Everton ndie aliyeanza kuliona lango la Spurs dakika ya 15 kipindi cha kwanza.
Nao Tottenham Hotspur walisimama na kuanza kutoa makosa yao na kuanza kusawazisha bao kupitia kwa Christian Eriksen dakika ya 21 na dakika za mwishoni za kipindi cha kwanza Spurs waliongeza bao na kutangulia kwa bao lililofungwa na Roberto Soldado na kuwa 2-1 dhidi ya Everton.
Mtanange huo ulimalizika kwa bao hizo 2-1 na Spurs kupanda juu hadi nafasi ya 7 kwenye msimamo wao wa Ligi kuu England. Vinara Chelsea bado wanaongoza juu kileleni wakiwa na pointi 33.
No comments:
Post a Comment