BUKOBA SPORTS

Tuesday, November 4, 2014

PREMIER LEAGUE: CRYSTAL PALACE 1 vs 3 SUNDERLAND: STEVEN FLETCHER AIPA USHINDI UGENINI SUNDERLAND!

Steven Fletcher aliiwezesha kupata Ushindi Sunderland kwa kuifunga Crystal Palace waliokuwa nyumbani Selhurst Park Bao 3-1 na kuisaidia kuiinua toka eneo hatari la kushuka Daraja la Ligi Kuu England.

Fletcher aliipa Sunderland Bao la kuongoza lakini Beki wao Wes Brown alijifunga mwenyewe na kuwapa Palace Bao la kusawazisha.
Jordi Gomez akaipa Sunderland Bao la Pili na mwishowe Fletcher akafunga Bao lake la pili na kuifanya Sunderland ishinde Bao 3-1.
Ushindi ni mtamu kwa Sunderland kwani katika Mechi yao iliyopita ya Ugenini walipigwa 8-0 na Southampton. 
Steven F. akishangilia baada ya kufunga moja bao zake usiku huuMashabikiKipa wa Sunderland Costel akiokoa mpira wa kichwa uliopigwa na ChamakhCrystal Palace's Fraizer Campbell celebrates their first goal with Joe Ledey and team matesCrystal Palace nao walipata bao la pekee na hapa wakishangilia.

No comments:

Post a Comment