
Msanii wa Bongofleva anayekuja kwa kasi katika mchakato wa kuchanganya nyimbo za asili na za kizazi kipya kutoka Bukoba,BK Sande.

Mwanamuziki mahiri kutoka Nchini Uganda Lady Mariam "Tindatine" (kulia) akiwa na Mwanamuziki wa Hapa Bukoba BK Sande wakijiandaa kutoa Burudani ya nguvu hii leo Alhamisi X-Mass kwenye Ukumbi wa Bukoba Club. Wanamuziki hao wanatarajia kutoa Burudani mchana na usiku katika Ukumbi huo wa Bukoba Ckub, Burudani ya Mchana itakuwa ni ya Watoto na Watu wazima nayo itaanza mchana mpaka jioni na Usiku ni shoo ya Watu wazima ambayo nayo itaenda mpaka majogoo.
Kiingilio katika shoo hiyo ya Mchana Watoto itakuwa ni Tsh.3,000/- na Wakubwa ni Tsh 5,000/- Msanii huyo mahiri kutoka Nchini Uganda aliyetamba na Wimbo wa Tindatine ambaye ni kwa mara yake ya kwanza Kuja hapa Bukoba wakati wa Sikukuu ya X-Mass amewataka Wakaazi wa Bukoba kujitokeza kwa wingi kushuhudia kile alichowaandalia kwa siku ya leo ya X-Mass, Na amewataka Watoto wa lika zote kuja kwani shoo yao itakuwa ni mchana usiku ni watu wazima tu.

Shoo ya Usiku italipiwa kwa VIP 10,000/- na Kawaida ni Tsh.5,000/-
Na Baada ya hapo kesho yake siku ya Ijumaa siku ya Boxing Day shoo hiyo itaamia katika Ukumbi wa hotel mpya ya NALPHIN HOTEL & NIGHT CLUB uliopo Wilayani Muleba. Usiku ambapo kiingilio kitakuwa ni Tsh. 15,000/ kwa VIP na Kawaida ni Tsh.10,000/-

Lady Mariam na BK Sande wakitokelezea..

Msanii wa Muziki BK Sande
No comments:
Post a Comment