BUKOBA SPORTS

Sunday, December 21, 2014

FULL TIME: LIVERPOOL 2 vs 2 ARSENAL, MARTIN SKRTEL AWANYIMA USHINDI GUNNERS!! ASAWAZISHA BAO DAKIKA ZA MWISHONI!

2-2!!!Martin Skrtel Aliiwezesha Liverpool kutoka sare na kugawana pointi moja moja na Arsenal baada ya kuifungia bao la kusawazisha na kutoka 2-2 leo kwenye mchezo wa Ligi kuu England.Liverpool wakipongezana na wao!Olivier Giroud Kipindi cha pili dakika ya 64 aliipachikia bao la pili Arsenal na kufanya 2-1 dhidi ya Wenyeji Liverpool baada ya kupata mpira kutoka kwa Santi Cazorla. Kipindi cha kwanza kilimalizika 1-1 timu zote mbili zikijipatia bao katika dakika za mwishoni mwa kipindi hicho cha kwanza.
Coutinho aliifungia bao safi Liverpool baada ya kupata pasi kutoka kwa Jordan Henderson katika dakika ya 45 kipindi cha kwana nao Arsenal waliweza kusawazisha katika dakika chache dakika ya za nyongeza za kipindi cha kwanza. Bao likifungwa na Mathieu Debuchy baada ya kupigwa frii kiki na kutokea gonga gonga ya kichwa kutoka kwa Mathieu Flamini.
Mpaka mapumziko ilikuwa ni 1-1 Arsenal wamesawazisha ndani ya dakika moja tu katika kipindi cha kwanza mwishoni.
Arsene Wenger na Brendan Rodgers wakisalimiana leo.

No comments:

Post a Comment