BUKOBA SPORTS

Saturday, December 13, 2014

MTANI JEMBE - FULL TIME: SIMBA 2 vs 0 YANGA, MASHABIKI WAPAGAWA UWANJANI TAIFA!


SIMBA leo imeendeleza ubabe dhidi ya Yanga katika mchezo wa Kampeni ya Nani Mtani Jembe baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 katika mchezo uliofanyika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Mchezo kama huo Desemba 21 mwaka jana Simba iliibuka na ushindi wa mabao 3-1, yaliyofungwa na Amis Tambwe na Awadh Juma.


Kocha wa Simba, Patrick Phir akisalimiana na kocha wa Yanga, Marcio Maximo kabla ya mchezo. (Picha zote na Francis Dande)

Emmanue Okwi akiomba dua wakati akiingia uwanjani.

Mgeni rasmi akisalimiana na wachezaji wa Yanga.

Mgeni rasmi akisalimiana na wachezaji waSimba.

Kikosi cha Yanga.

Kikosi cha Simba.
Kocha wa Yanga MarcioMaximo akitafakari.
Mchezo huo ulichezeshwa na mwamuzi Jonesia Rukyaa, ikiwa ni mara ya kwanza katika historia mechi ya Simba na Yanga mwanamke kupuliza filimbi.Mfungaji wa bao la tatu katika mchezo kama huo mwaka jana, Awadhi Juma, ndiye jana alifunga bao la kwanza dakika ya 30 akimalizia mpira wa adhabu uliopigwa na Emmanuel Okwi na kutemwa na kipa Deogratius Munishi ‘Dida’.
Bao hilo lilionekana kuwachanganya sana wachezaji wa Yanga na kujikuta wakicheza hovyo, hali iliyosababisha wafungwe bao la pili dakika ya 40, mfungaji akiwa Elius Maguli.
Maguri alifunga bao hilo baada ya mpira wa kichwa aliopiga kugonga nguzo ya goli na kurejea uwanjani na kumkuta mfungaji aliyeukwamisha wavuni na kumuacha Dida akigaagaa.
Yanga ingeweza kupata bao la mapema kutokana na kufanya mashambulizi ya kushtukiza baada ya kuanza mchezo huo, lakini umalizijia haukuwa mzuri.

Mshambuliaji wa Simba, Emmanuel Okwi akiwa amenyanyua juu Kombe la Ubingwa wa mechi ya Nani Mtani Jembe msimu wa pili uliofanyika leo kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Simba imeshinda 2-0.
Waziri wa Habari Vijana Utamaduni na Mchezo, Dk. Fenella Mukangala akimkabidhi nahodha wa Simba, Emmanuel Okwi Kombe la Ubingwa wa mechi ya Nani Mtani Jembe.

Wachezaji wa Simba wakishangilia ushindi wa timu yao.
 Umati wa mashabiki wa Yanga.
Umati wa mashabiki wa Simba.
Mashabiki wa Simba wakiwa wamebeba mfano wa jeneza kuwakejeli watani zao.
Beki wa Yanga, Nadir Haroub 'Canavaro'
Beki wa Yanga, Kelvin Yondan akimiliki mpira.
Mwamuzi wa mchezo huo akimuonyesha kadi ya njano mshambuliaji wa Simba, Simo Serunkuma.
Kpah Sherman akiokoa moja ya hatari langoni mwake huku Elius Maguri akimzonga.
 Mshambuliaji wa Simba Emmanule Maguri akichuana na beki wa Yanga, Nadir Haroub.
Wachezaji wa Simba wakishangilia bao lao la kwanza.
 Hassan Isihaka (kushoto) na Ramadhani Singano 'Messi' wakishangilia bao la kwanza la timu yao.
Beki wa Yanga, Oscar Joshua akimtoka Elius Maguri wa Simba.
Shabiki wa Yanga akipata msaada baada ya kuzimia jukwaani.
 Mashabiki wa Simba wakiwa na bango lenye idadi ya mabao waliyowahi kufungwa Yanga.
Leo ni 2-0.....
Burudani zikitolewa uwanjani.
 Mashabiki wakitolewa uwanjani baada ya kuzimia.
 Hali ilikuwa ngumu kwa mashabiki mpaka baadhi yao kuzimia.
Huduma ya kwanza kwa waliozimia ikitolewa.
 Beki wa Yanga, Kpah Sherman akichuana na beki wa Simba, Hassan Isihaka.
 Danny Mrwanda akiwa ameshika kichwa baada ya kukosa bao la wazi.
Ivo Mapunda akiokoa moja ya hatari langoni mwake.

 Simon Msuva akichuana na Issa Rashid.
Ivo Mapunda (katikati) akishangilia ushindi na wenzake.
Wachezaji wa Yanga wakiwa na huzuni baada ya kumalizika kwa mchezo.
Yanga wakiwa vichwa chini.
 Medali za washindi.


Mshambuliaji mpya wa Yanga, raia wa Liberia, Kpah Sherman mara kadhaa alijaribu kufurukuta lakini alikosa ushirikiano wa kutosha.
Simba nayo licha ya ushindi huo, lakini washambuliaji wake wakiongozwa na Simon Sserunkuma, Elias Maguli na Emmanuel Okwi walipata nafasi za kufunga, lakini walishikwa na kigugumizi cha miguu kila waliposogea eneo la hatari.
Kipindi cha pili, Yanga ilipata pigo baada ya Sherman kuumia, hivyo kutolewa nje na nafasi yake kuchukuliwa na Mrisho Ngassa.
Dakika ya 62, Danny Mrwanda aliyeingia kipindi cha pili badala ya Andrey Coutinho nusura aipatie Yanga bao, baada ya mpira aliopiga kuokolewa na beki Hassan Isihaka, wakati kipa Ivo Mapunda hayupo golini.
Dakika ya 67 Sserunkuma akiwa katika nafasi nzuri ya kufunga, shuti lake lilipaa juu kidogo ya lango la Yanga, huku tayari baadhi ya mashabiki wa Simba wakianza kuinuka wakiamini amefunga.





Simba: Ivo Mapunda, Nassor Masoud, Mohammed Hussein/Issa Rashid,
Hassan Isihaka, Juuko Murishid/Joseph Owino, Jonas Mkude, Ramadhani Singano/Said Ndemla, Awadh Juma, Elius Maguri/Danny Sserunkuma, Simon Sserunkuma/Shaaban Kisiga na Emmanuel Okwi.

Yanga: Deogratius Munishi, Abdul Juma/Hussein Javu,Oscar Joshua, Nadir Haroub, Kelvin Yondani, Mbuyu Twite/Hassan Dilunga, Haruna Niyonzima, Emerson Roque/Salum Telela, Simon Msuva, Kpah Sherman/Mrisho Ngassa na Andrey Coutinho/Danny Mrwanda.

No comments:

Post a Comment