BUKOBA SPORTS

Wednesday, December 24, 2014

WACHEZAJI WA MANCHESTER UNITED WAPEWA NAFASI KULA X-MASS NA FAMILIA ZAO. VAN GAAL APITISHA JAMBO HILO!

Wachezaji wa Manchester United wamepewa ofu toka Mazoezini Siku ya Krismasi baada ya Meneja wao Louis van Gaal kusema ni muhimu Wachezaji hao kuwa na Familia zao wakati wa Krismasi.
Siku ya pili baada ya Krismasi, Ijumaa Siku ya Boksingi, Man United watakuwa kwao Old Trafford kucheza na Newcastle katika Mechi ya Ligi wakisaka kutofungwa katika Mechi zao 8 za Ligi baada ya kushinda 6 na Sare 1.
Huko England, tofauti na Nchi nyingine za Ulaya kama vile Spain, Italy na Germany ambako Ligi husimama kupisha Krismasi na Mwaka Mpya, Ligi huendelea wakati huo na Timu huwa Mazoezini Siku ya Krismasi ili kujitayarisha Mechi za Siku ya Pili, Siku ya Boksingi.
Van Gaal, ambae ni mara ya kwanza kufanya kazi kama Meneja Siku ya Krismasi, amesisitiza Mazoezi si muhimu sana kwa kusema: “Naamini Watu, mazingira ni muhimu. Wao watakuwa na furaha zaidi wakiwa Makwao na Wake na Watoto zao. Wakirudi, naamini, watajitolea kwa moyo wote kumshinda Mpinzani!”

No comments:

Post a Comment