
KUNDI B la Mashindano ya Mataifa ya Afrika, AFCON 2015, limecheza Mechi zao za mwisho ambazo zote mbili ziliisha kwa Sare ambazo zimewanufaisha Tunisia na Congo DR kutinga Robo Fainali huku Cape Verde na Zambia wakitupwa nje.
Zambia ilikuwa na matumaini ya kuibuka na ushindi katika mchezo huo lakini hali iliwaendea ndivyo sivyo na kujikuta ikipoteza nafasi nyingi za wazi na kushindwa kukwamisha mpira wavuni.
Katika mchezo mwingine wa kundi hilo timu ya taifa ya Tunisia imeweza kutoshana nguvu na DR Congo baada ya kufungana goli moja kwa moja na kufanikiwa kufuzu katika hatua inayofuata ya michuano hiyo inayoendelea kutimua nchini Equatorial Guinea.
Ahmed Akaichi akishangilia bao lake dhidi ya Congo
Kipa wa Congo Robert Muteba Kidiaba akikabana koo na Wahbi Khazri wa Tunisia.
Mchezaji wa Congo Jeremy Bokila kwenye patashika ya bao la kusawazisha...
No comments:
Post a Comment