Ili kuleta umoja katika mkoa kwa watoto wa kike na kiume Jambo Bukoba kuanzia mwaka 2012 ilianzisha bonanza la michezo kila mwisho wa mwaka la kuwaunganisha watoto kutoka shule mbalimbali mkoani Kagera ili waweze kushirikiana pamoja kimichezo na kujenga kujiamini kwa pamoja.
Bonanza la michezo la Jambo Bukoba mwaka 2014 litafanyika mwaka huu 30 Januari, 2015 na kushirikisha Wilaya zote za mkoa wa Kagera pamoja na mwanzilishi wa Jambo Bukoba akiambatana na wenzake kutoka nchini Ujerumani.
Bonanza la michezo la Jambo Bukoba litafanyika katika viwanja vya Gymkhana Manispaa ya Bukoba kuanzia saa 2:00 asubuhi, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Kagera ikishirikiana shirika la Jambo Bukoba wanawakaribisha wananchi wote kuhudhuria na kushiriki katika bonanza hilo. Kagera. Vilevile ili kuhakikisha watoto wanaendelea kupata elimu nzuri Jambo Bukoba imeanza kukarabati miundombinu mbalimbali katika baadhi ya shule za msingi mkoani hapa.
Miundombinu hiyo ni pamoja na madarasa ambayo yameharibika na kuhitaji ukarabati, kujenga matundu ya vyoo vipya pamoja na kukarabati ofisi za walimu ambazo ziko katika hali mbaya ili kuwarahisishia walimu katika kutekeleza majukumu yao vizuri ya ufundishaji.
Lengo la mwanzilishi wa Jambo Bukoba Bw. Mulokozi ni kupunguza kasi ya watoto wa kike kuanzisha mahusiano ya kimapenzi wakiwa wadogo, pia kupunguza unyanyapaa wa wtoto wa kiume kwa watoto wa kike ambapo Jambo Bukoba imepunguza tatizo hilo kwa kiasi kikubwa mkoani Kagera.
No comments:
Post a Comment