BUKOBA SPORTS

Tuesday, January 27, 2015

CAPITAL ONE CUP: NUSU FAINALI LEO JUMANNE USIKU MARUDIANO STAMFORD BRIDGE CHELSEA vs LIVERPOOL

Baada ya kutoka Sare 1-1 huko Anfield katika Mechi ya Kwanza ya Nusu Fainali ya Kombe la Ligi, sasa maarufu kama Capital One Cup, Chelsea na Liverpool zitarudiana Uwanjani Stamford Bridge Jumanne Usiku Januari 27.
Katika Mechi ya Kwanza iliyochezwa Wiki iliyopita, Chelsea walitangulia kufunga kwa Penati ya Eden Hazard katika Dakika ya 18 na Raheem Sterling kuisawazishia Liverpool kwenye Dakika ya 59.
Kwenye Nusu Fainali, Kanuni muhimu inayotumika ni ile ya kupata Mshindi ikiwa Timu zìtakuwa Sare na pia kufungana kwa Magoli sawa katika Mechi zao 2 baada ya Dakika 90.
Hali ikiwa hivyo, bila ya kuhesabu Magoli ya Ugenini, utachezwa Muda wa Nyongeza wa Dakika 30 na baada ya muda huo, ikiwa Mechi bado ni Sare, basi ile Sheria ya Bao la Ugenini kuhesabika Mawili ndiyo itatumika.
Na endapo, wakati huo, hata ikitumika Sheria ya Bao la Ugenini kuwa Mawili bado Timu zinabaki Sare, Mshindi atapatikana kwa Mikwaju ya Penati 5.
Katika Nusu Fainali nyingine ambayo Mechi ya kwanza ilichezwa pia Wiki iliyopita huko White Hart Lane, Tottenham iliifunga Sheffield United Bao 1-0 kwa Bao la Penati iliyotolewa Dakka ya 75 baada ya Jay McEveley kuushika Mpira na Andros Townsend kupiga Penati hiyo na kufunga.

Marudiano ya Sheffield United na Tottenham ni hapo Jumatano Januari 28 Nyumbani kwa Sheffield.

No comments:

Post a Comment