BUKOBA SPORTS

Tuesday, January 27, 2015

UHAMISHO: PARIS SAINT GERMAIN KUMBEBA ADNAN JANUZAJ??


Wakala wa mchezaji kinda wa Manchester United Adnan Januzaj, De Vriese ametoboa siri kuwa Manchester United chini ya kocha Louis Van Gaal imekaa ombi kutoka kwa miamba ya soka nchini ufaransa Paris Saint Germain kumsajili mchezaji huyo katika dirisha dogo la usajili.

Januzaj mwenye umri wa miaka kumi na tisa, amekuwa akiangaika kupata namba katika kikosi cha kwanza cha kocha Louis Van Gaal lakini ameishia kucheza mechi kumi na tatu pekee katika mashiandano yote msimu huu.
"Ndio,PSG wameonyesha nia ya kumsajili Januzaj kipindi hiki," wakala De Vriese aliliambia Gazeti la Foot Mercato.

Januzaj anamkataba wa kuitumikia Manchester United mpaka mwezi June 2018.

No comments:

Post a Comment