WENYEJI wa Mashindano Australia wamefanikiwa kutwaa Kombe la Mataifa ya Asia, Asian Cup, baada ya kuichapa South Korea Bao 2-1 kwenye Fainali iliyochezwa Dakika 120 Mjini Sydney.
Hadi Dakika 90 kumalizika kwa Bao 1-1.
Australia walitangulia kufunga katika Dakika ya 45 kwa Bao la Luongo na Korea kusawazisha kwenye Dakika ya 92 kwa Bao la Son Heung-min 9.
Katika Robo Saa ya kwanza ya Dakika za Nyongeza 30, James Troisi aliipa Australia Bao lao la ushindi katika Dakika ya 105.
Jana Ijumaa ilichezwa Mechi ya kusaka Mshindi wa 3 na United Arab Emirates kuifunga Iraq 3-2.
No comments:
Post a Comment