BUKOBA SPORTS

Monday, January 26, 2015

FA CUP: DROO YA RAUNDI YA 5 KUFANYIKA LEO JUMATATU USIKU.

Droo ya kupanga Mechi za Raundi ya 5 ya Kombe hili Kongwe kupita yote Duniani itafanyika Jumatatu Usiku.
Droo hiyo itapanga Mechi 8 za Raundi ya 5 ambazo zitachezwa Wikiendi ya Februari 14 na 15 na Washindi wake kutinga Raundi ya 6 ambayo ndio Robo Fainali.
Vigogo ambao watakasokena kwenye Droo hiyo baada ya kutolewa hapo Jana ni pamoja na Mabingwa wa England, Manchester City, Vinara wa Ligi Kuu England, Chelsea, Tottenham, Southampton pamoja na Timu nyingine kadhaa za Ligi Kuu England.

Mtangazi wa BBC, Gary Lineker, ambae aliwahi kubeba FA CUP Mwaka 1991 wakati akiichezea Tottenham Hotspur, ndie atakuwa akiokota Mipira yenye Majina ya Timu toka kwenye Chungu wakati wa Droo hiyo itakayoanza Saa 4 Dakika 20 Usiku Jumatatu Januari 26.


NAMBA ZA DROO:
1. Crystal Palace
2. Cambridge United au Manchester United
3. Blackburn Rovers
4. Bradford City
5. Derby County
6. Preston North End au Sheffield United
7. West Bromwich Albion
8. Aston Villa
9. Reading
10. Liverpool or Bolton
11. Leicester City
12. Arsenal
13. Rochdale au Stoke City
14. Sunderland au Fulham
15. West Ham
16. Middlesbrough



TAREHE ZA RAUNDI:-
-Raundi ya 4: 24 Januari 2015
-Raundi ya 5: 14 Februari 2015
-Raundi ya 6: 7 Machi 2015
-Nusu Fainali: 18 & 19 Aprili 2015
-Fainali: 30 Mei 2015

No comments:

Post a Comment