BUKOBA SPORTS

Sunday, January 25, 2015

LA LIGA: ELCHE 0 - 6 BARCELONA, LIONEL MESSI NA NEYMAR WATUPIA MBILI MBILI WAKIWACHAKAZA MTU 10 ELCHE!

Pongezi...BARCELONA wameitwanga Elche Bao 6-0 katika Mechi ya La Liga waliyocheza Ugenini Usiku huu na kuwakaribia Vinara Real Madrid wakiwa Pointi 1 nyuma yao ingawa wao wamecheza Mechi 1 zaidi.
Mapema hii Leo, Real nao walipata ushindi wa Ugenini walipoipiga Cordoba Bao 2-1.

Bao za Barca hii Leo, waliocheza na Mtu 10 Elche tangu Dakika ya 57 baada ya Fayçal Fajr kupewa Kadi Nyekundu, zilifungwa na Gerrard Pique, Dakika ya 35, Lionel Messi, Dakika za 55 na 88 moja likiwa Penati, na Neymar aliefunga Dakika za 69 na 71 huku Pedro akihitimisha Mabao katika Dakika za Nyongeza.

No comments:

Post a Comment