Inaaminika City watalipa Pauni Milioni 30 kumnunua Bony lakini Fedha hizo zitalipwa kwa awamu kwa sababu ya City kubanwa na UEFA kuhusu FFP [Financial Fair Play] inayotaka Klabu zijiendeshe kwa Mapato yao wenyewe bila kutegemea ruzuku toka kwa Wamiliki wao Matajiri.
Inatatarajiwa kuwa Bony, mwenye Miaka 26, atasaini Mkataba wa Miaka Minne na kulipwa Mshahara wa zaidi ya Pauni 100,000 kwa Wiki akiwa huko Etihad.
City wamelazimika kumnunua Bony baada kuumia kwa Straika wao mkubwa Sergio Aguero ambae amewafungia Bao 19 Msimu huu huku Mastraika wao wengine, Stevan Jovetic na Edin Dzeko, pia wakikumbwa na Majeruhi na pia kuwa Wafungaji hafifu wakifunga jumla ya Bao 11 tu kati yao.
Kwa Mwaka mzima wa 2014, Bony alifunga jumla ya Mabao 20 ambayo ni mengi kupita Straika yeyote wa Ligi Kuu England.
No comments:
Post a Comment