
Na Faustine Ruta, Mwanza
AMAVUBI WATUA MWANZA LEO HII, WAFANYA MAZOEZI KATIKA UWANJA WA CCM KIRUMBA.
Timu ya Taifa ya Rwanda (Amavubi) Imewasili leo Jijini Mwanza, Januari 21 kwa ajili ya mechi ya kirafiki ya kimataifa dhidi ya Taifa Stars Maboresho itakayochezwa kesho kwenye Uwanja wa CCM Kirumba hapa Mjini Mwanza.
Amavubi imetua na msafara wa watu 26, wakiwemo wachezaji, benchi la ufundi na viongozi na kufikia kwenye hoteli ya JB Belmont.

Wachezaji baadhi wa Timu ya Amavubi ya Nchini Rwanda walipa picha ya pamoja kwenye Uwanja wa CCM Kirumba Jijini Mwanza jioni ya leo, Tayari kwa Mtanange wa kirafiki wa Kitaifa kesho na Timu ya Hapa Nchini ya Taifa Stars Maboresho.

(Katikati) ni Haruna Niyonzima akitokelezea kwenye Picha pamoja.

Haruna Niyonzima

Haruna Niyonzima akiwa na VIongozi wa Timu hiyo Amavubi

Haruna Niyonzima

Picha ya Pamoja

Mchezaji wa Timu ya Amavubi akitokelezea kwenye lango kwenye Uwanja wa CCM Kirumba.

Hatari tupu!! Kesho ni Taifa starz Maboresho VS Amavubi

Wachezaji wa Timu ya Amavubi ya Nchini Rwanda wakiwa wamekaa kwenye Uwanja CCM Kirumba huku wakiunda mbinu ya kuifunga Timu ya Taifa Stars Maboresho kwenye Uwanja wa CCM Kirumba Mwanza.

Mwandishi wa www.bukobasports.com nae alipata picha ya pamoja na Wachezaji wa Rwanda (AMAVUBI) leo hii jioni kwenye Uwanja wa CCM Kirumba Jijini Mwanza.
No comments:
Post a Comment