COPA DEL REY: USIKU HUU NI ROBO FAINALI YA KWANZA NOU CAMP - BARCELONA vs ATLETICO MADRID, DIEGO SIMEONE KUIBANA BARCA NA MESSI WAO!
Kocha wa Atletico Madrid, ametamba kuwa ameshapata dawa ya kuziumiza Barcelona na Real Madrid wakati Jumatano Usiku watatua Nou Camp kucheza na Barcelona katika Mechi ya kwanza ya Robo Fainali ya Kombe la Mfalme wa Spain, Copa del Rey.
Msimu uliopita, Diego Simeone aliiongoza Atletico Madrid kumaliza ngebe za Barca na Real za kutwaa Ubingwa wa Spain kwa Miaka 10 baada ya kutoka Sare 1-1 na Barca Uwanjani Nou Camp katika Mechi ya mwisho ya La Liga na wao kutwaa Ubingwa.
Kwenye Raundi iliyopita ya Copa del Rey Wiki iliyopita, Atletico Madrid waliwabwaga Mahasimu wao wakubwa Real Madrid, ambao ndio walikuwa Mabingwa Watetezi, kwa Jumla ya Bao 4-2 katika Mechi mbili.
Atletico waliishinda Real Mechi ya kwanza 2-0 Nyumbani kwao Vicente Calderon na kutoka Sare 2-2 huko Santiago Bernabeu.
Hata hivyo, Atletico walibamizwa Bao 3-1 na Barca huko Nou Camp kwenye Mechi ya La Liga Mapema Mwezi huu.
Licha ya kipigo hicho, Diego Simeone, Raia wa Argentina, ametamba na kuzichambua Barca na Real: “Barca wanatumia nafasi ndogo Uwanjani na Real wanatumia nafasi kubwa na kutumia kaunta ataki. Ni ngumu kushindana na Barca na Real lakini tumepata dawa kwa kucheza kwa kubidii na nguvu na kufanya Gemu iwe ngumu mno kwao!”
Tangu achukue wadhifa Atletico Miaka Mitatu iliyopita, Diego Simeone ameweza kutwaa Ubingwa wa La Liga mara moja, Europa Ligi moja, Copa del Rey moja na kufika Fainali ya UEFA CHAMPIONS LIGI.
No comments:
Post a Comment