BUKOBA SPORTS

Saturday, February 14, 2015

BARNABA BOY NA AMINI WATINGA RADIO KASIBANTE 88.5 FM RADIO BUKOBA, TAYARI KWA KUTOA BURUDANI LEO VALENTINE DAY LINA'S NIGHT CLUB.

Mwanamuziki anayefanya vizuri katika tasnia ya muziki nchini Elias Barnabas ‘Barnaba’ akiimba moja ya wimbo wake Ndani ya Studio Radio Kasibante 88.5 FM  huku akipiga Gitaa lake..

Mzee wa Robo saa Amini akitokelezea leo wakati anazungumza na Wananchi wa Bukoba Kupitia Radio Kasibante  88.5 FM leo ambapo usiku huu watakuwa pamoja na Barnaba kwenye Ukumbi wa Lina's Night Club kutoa Burudani ya Nguvu na Special kwa Siku ya Wapendanao "Valentine Day" Picha na Faustine Ruta wa bukobasports.com
Msanii Elias Barnabas ‘Barnaba’ akifanya yake..

Mc Jerry kutoka Shemeji Investment ambaye ni mmoja wa Waandaji wa Show ya leo akitoa ufafanuzi wa Tiketi kupitia Radio Kasibante Fm.Mc Jerry na Barnaba
Msanii wa bongo flava aliyefanya Vyema kwenye Jumba la (THT) Tanzania House of Talent, Amini Mwinyimkuu na (kulia) ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Zachwa Investment ambaye ndie Mwandaaji akishirikiana na Shemeji Investment kuandaa Show bab kubwa ambayo itapambwa na Wasanii hao kutoka Jijini Dar es salaam leo siku ya Valentine Day kwenye Ukumbi wa Lina's Night Club. Hapa walikuwa kwenye Chumba cha Radio kasibante wakifanya mahojiano na Mtangezaji Nicolaus Ngaiza (hayupo pichani). Picha na Faustine Ruta wa bukobasports.com
Faustine Ruta wa bukobasports.com(kushoto) akiwa na Msanii wa Bongo Flava Amini nje ya Jengo la Kasibante FM Radio leo hii jioni.

No comments:

Post a Comment