BUKOBA SPORTS

Saturday, February 14, 2015

BAYERN MUNICH 8 vs 0 HAMBURG SV, THOMAS MULLER, ARJEN ROBBEN NA WENZAKE WAANGUSHA KIPIGO CHA MWIZI NA CHA KUFUNGULIA MWAKA 2015

Mbele ya Mashabiki  75,000  Timu ya Bayern Munich imewachinja bao 8-0 Timu ya Hamburg SV bila kujitetea katika mchezo huo uliomalizika muda mchache uliopita.

Wafungaji ni kama wafuatavyo:
Thomas Müller 21' PEN •
Mario Götze 23' •
Arjen Robben 36' •
Arjen Robben 47' •
Thomas Müller 55' •
Robert Lewandowski 56' •
Franck Ribéry 69' •
Mario Götze 88'

Mabingwa Watetezi wa Bundesliga, Bayern Munich leo wakiwa kwao Allianz Arena wameitandika Hamburger SV Bao 8-0 katika Mechi ya Bundesliga.
Bao za Bayern zilifungwa na Thomas Muller, Bao 2 moja kwa Penati, Arjen Robben, Bao 2, Mario Götze, Bao 2, wakati Franck Ribbery na Robert Lewandoeski walifunga Bao 1 kila mmoja.
Nayo Timu ya Pili, VfL Wolfsburg, wakicheza Ugenini, waliichapa Bayer 04 Leverkusen Bao 5-4 huku Wachezaji wao Bas Dost akipiga Bao 4 na Naldo akifunga moja wakati Bao za Leverkusen zilifungwa na Son Heung-Min, Bao 3, na Bellarabi K. Bao 1.

Matokeo haya yamewabakisha Bayern Munich kuongoza Ligi wakiwa Pointi 8 mbele ya VfL Wolfsburg.

No comments:

Post a Comment