BUKOBA SPORTS

Saturday, February 14, 2015

USAILI WA WACHEZAJI WA NSSF-REAL MADRID SPORTS ACADEMY WAANZA JIJINI DAR ES SALAAM

Msimamizi wa zoezi la kuandikisha vijana wenye vipaji wa kucheza soka, Chacha Samburu, (kulia) akimwelekeza mzazi wa Omar Adam (katikati) mama Kinara Godwin (kushoto) jinsi ya kujaza fomu kwenye usajili unaosimamaiwa na mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii kupitia Mradi wake wa Kituo cha Mpira wa Miguu kijulikanacho kama NSSF-REAL MADRID Sports kwenye uwanja wa Karume jijini Dar es Salaam
Mkurugenzi wa Operesheni wa NSSF, Crescentius Magori akizungumza na baadhi ya wasimamizi wa zoezi la usaili
Mkurugenzi wa Operesheni wa NSSF, Crescentius Magori (KULIA) akiteta jambo na mwakilishi wa Real Madrid (kushoto) wakati usajili ukiendelea
MFUKO wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii kupitia Mradi wake wa Kituo cha Mpira wa Miguu kijulikanacho kama NSSF-REAL MADRID Sports Academy wameanza usajili wa kusaka vijana wenye vipaji watakao jiunga na kituo hicho kwenye uwanja wa Karume jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na waandishi wa habari leo, Mkurugenzi wa Operesheni wa NSSF, Crescentius Magori alisema kuwa anashukuru wazazi kwa kujitokeza kwa wingi kwenye uandikishaji wa kuwabaini vijana ambapo wana vipaji vya mpira wa miguu.
“Uandikishaji huu utahusisha vijana wa kiume waliozaliwa kati ya 2001 hadi 2002 June, na unafanyika bure kuanzia leo (jana) na kesho na utaendelea wiki ijayo siku ya jumamosi na jumapili kuanzia saa maoja asubuhi hadi saa tisa aliasiri”, alisema Magori.

Zoezi la kuandikisha halina gharama zozote bali kila mmoja atatakiwakuja na picha mbili za passport size na cheti cha kuzaliwa na mzazi wake au mlezi wake ili kujaza fomu maalum ambayo atapewa namba ya ushiriki.


Pia Magori alisema kuwa vijana ambao watachaguliwa kujiunga na kituo chao pamoja na kufundishwa soka pia watakuwa wnaafundishwa masomo ya elimu ya sekondari kulingana na mtaala wa elimu ya Tanzania ili wawe wazuri katika soka na kichwani pia.


Zoezi hili linalengo la kupata vijana 500 ambao watakaofanyiwa majaribio na wataalamu kutoka Klabu ya Real Madrid na hatimaye kupatikana vijana 30 amabo ndio wataingia katika shule maalum ya mafunzo kwa awamu ya kwanza.


Shirika la NSSF linatoa wito kwa vijana kujitokeza kwani ni fursa kwao ya kuweza kujiendeleza kimichezo na kujiajiri kupitia michezo.

No comments:

Post a Comment