
Katika mchezo huo ambao ulitawaliwa na vituko vya mashabiki wa Friends Rangers, ulishuhudia African Sports wakijipatia bao la kwanza dakika ya 12 na kiungo mshambuliaji, Ramadhan Msheli baada ya kuwatoka mabeki wa Friends Rangers.
Baada ya bao hilo wachezaji wa Friends Rangers walijitahidi kusawazisha bao lakini walijikuta wakienda mapumziko wakiwa nyuma kwa bao hilo moja
Kipindi cha pili kilianza kwa timu zote kufanya mabadiliko ambayo yaliongeza uhai kwa Friends Rangers na kujikuta wakipata bao dakika ya 46 lililofunga na mshambuliaji Ahmad Abas kwa shuti la mbali akiwa nje ya eneo la penati.
African Sports
African Sports baada ya kuona Friends Rangers wamesawazisha walicharuka na kuanza kuliandama lango lao na kufanikiwa kupata bao la ushindi lililofungwa na mshambuliaji James Mendi baada ya kuunganisha krosi ya Ally Ramadhan.
Akizungumza baada ya mchezo, kocha wa African Sports, Joseph Lazaro, alisema anawashukuru wachezaji, benchi la ufundi pamoja na uongozi kwa ushirikiano walionesha hadi kufanikisha timu kupanda daraja.
“Nawashukuru wachezaji kwa usikivu na ushirikiano wao tangu tulipoanza ligi na uongozi kwani umesaidia timu kufanya vizuri na nawahakikishia mashabiki wa Tanga kuwa tuna timu nzuri ambayo inakwenda kupambana ligi kuu na siyo kwamba tunaingia na kutoka”, alijigamba Lazaro.
Timu ya Majimaji ya Songea imeungana na African Sports kupanda ligi kuu kwa kundi A kwa msimu ujao huku timu ya Villa Squad ikishuka daraja la pili baada ya kumaliza ligi ikishikilia mkia kwa kundi A ikiwa na pointi 14.
Benchi la Friends Rangers
Michezo ya kundi B inatarajiwa kumalizika wikiendi ijayo ambapo Mwadui FC imeshapanda ikiwa na pointi 43 japo ina mchezo mmoja na kuacha ushindani kwa timu za Toto African yenye pointi 39 na JKT Oljoro 41, kila moja ikiwa imebakia na mchezo mmoja na kuicha Green Warriors ikihesabiwa kuwa imeshuka daraja baada ya kuwa ina pointi 11.
No comments:
Post a Comment