BUKOBA SPORTS

Thursday, February 19, 2015

COASTAL UNION WAIFUATA NDANDA NANGWANDA MTWARA

TIMU ya Coastal Union ya Tanga imeondoka mkoani hapa leo asubuhi kuelekea Mkoani Mtwara kwa ajili ya mechi yao ya Ligi kuu Tanzania Bara dhidi ya Ndanda SC itakayochezwa Jumamosi wiki hii.
Coastal Union ambayo mechi yao iliyopita dhidi ya Mbeya City iliyochezwa kwenye Uwanja wa CCM Mkwakwani haikupata matokeo mazuri sana baada ya kulazimishwa sare hivo itaingia kwenye mechi hiyo mithili ya mbogo aliyejeruhiwa msituni.
Akizungumzia maandalizi ya kuelekea mchezo huo, Kocha Mkuu wa Coastal Union, Mkenya James Nandwa alisema kuwa kikosi chake kimeimarika zaidi baada ya kuyafanyia kazi kwa asilimia kubwa mapungufu yaliyojitokeza mechi iliyopita.

 Alisema kuwa dhamira yake kubwa ni kuhakikisha kikosi hicho kinaibuka na ushindi kwenye mchezo huo ambao unatazamiwa kuwa na upinzani mkubwa kutokana na kila timu msimu huu kuonekana kujiimarisha vilivyo kwa ajili ya kupata matokeo mazuri.
"Kikosi changu kipo imara kuweza kuwakabili Ndanda SC ikiwemo kuhakikisha tunapata matokeo mazuri hii inatokana na maandalizi kabambe tuliyoyafanya hasa kubwa kurekebisha baadhi ya maeneo kwenye kikosi hiki " Alisema Kocha Nandwa.
Alisema kuwa mipango yake hivi sasa ni kukiwezesha kikosi cha timu hiyo kuweza kufanya vizuri kwenye mechi zao zijazo ili kuweza kusogea kwenye nafasi za juu kwenye msimamo wa Ligi kuu hapa nchini.
Msafara wa Coastal Union uliondoka leo mkoani hapa kuelekea mkoani Mtwara unaongozwa na mjumbe wa Kamati ya Utendaji , Albert Peter ambapo baada ya kuwasili Mkoani Mtwara utafanya mazoezi.



RATIBA:LIGI KUU VODACOM
Jumamosi Februari 21
Kagera Sugar vs Polisi Moro
Ndanda vs Coastal Union
Mgambo Shooting vs Mtibwa Sugar

Jumapili Februari 22

Mbeya City vs Yanga
Stand United vs Simba

Azam FC vs Tanzania Prisons
Jumamosi Februari 28
Mbeya City vs Ruvu Shooting
Mgambo Shooting vs Coastal Union
Simba vs Tanzania Prisons
Stand United vs Kagera Sugar

No comments:

Post a Comment