BUKOBA SPORTS

Tuesday, February 3, 2015

DIRISHA DOGO LA UHAMISHO KUFUNGWA, KOCHA WA QPR HARRY REDKNAPP AJIUZULU! SABABU NI KUFANYIWA OPERESHENI YA GOTI!


Harry Redknapp amejiuzulu kama Meneja wa QPR ambayo iko Nafasi ya Pili toka mkiani.
Redknapp, mwenye Miaka 67, alitaja sababu ya kujiuzulu ni kutakiwa kufanyiwa operesheni ya Goti lake.
Ameeleza: “Kwa bahati mbaya, ninatakiwa kufanyiwa operesheni ya Goti. Na kama siwezi kutumikia kwa Asilimia 100 ni bora mwingine ashike hatamu.”
Redknapp aliteuliwa kuwa Meneja wa QPR Novemba 2012 lakini ikateremka Daraja na Msimu uliopita akaipandisha tena kurejea Ligi Kuu England.
Uongozi wa QPR wamesema Timu yao sasa itasimamiwa kwa muda na Mkuu wao wa Soka, Les Ferdinand, na Kocha wa Vijana Chris Ramsey.

Harry Redknapp amejiuzulu kuifundisha Queens Park Rangers baada ya kuona hataweza kuiongoza kwa Muda Timu hiyo kutokana na hali yake ya Afya kuhitaji kufanyiwa operesheni ya Goti.
Queens Park Rangers wameshindwa kijitetea katika Vipigo 11 vikiwemo hata vya Uwanjani kwao Lofus Road

No comments:

Post a Comment