BUKOBA SPORTS

Tuesday, February 3, 2015

FA CUP: MARUDIANO - MANCHESTER UNITED vs CAMBRIDGE UNITED USIKU HUU OLD TRAFFORD

Manchester United, ambao wao pamoja na Mabingwa Watetezi Arsenal, ndio wanashika Rekodi ya kutwaa FA CUP mara nyingi, mara 11 kila mmoja, Jumanne Usiku wanarudiana na Cambridge United Uwanjani Old Trafford baada ya kutoka 0-0 katika Mechi ya kwanza iliyochezwa Abbey Stadium Nyumbani kwa Timu hiyo ya Daraja la Chini, Ligi 2. Hii ni Mechi ya Raundi ya 4 ya FA CUP na Mshindi atatinga Raundi ya 5 na kucheza na Mshindi kati ya Preston au Sheffield United ambao nao wanarudiana leo Jumanne.
Mara ya mwisho na pekee kwa Cambridge United kucheza Uwanjani Old Trafford ni Mwaka 1991 walipotwangwa Bao 3-0 kwenye Kombe la Ligi ambalo sasa linaitwa Capital One Cup.

No comments:

Post a Comment