BUKOBA SPORTS

Monday, February 2, 2015

UHAMISHO: SIKU YA MWISHO - JUAN CUADRADO ATUA CHELSEA, SCHURRLE NA MOHAMED SALAH WAONDOKA KLABUNI CHELSEA... ZAHA WA MAN UNITED ARUDI CRYSTAL PALACE, YAKUBU AREJEA ENGLAND!

Vinara wa Ligi Kuu England, Chelsea, hatimaye wamekamilisha Usajili wa Mchezaji wa Kimataifa wa Colombia, Juan Cuadrado, kutoka Fiorentina baada ya kukwama kutokana na Dili za Uhamisho za Wachezaji wao Andre Schurrle na Mohamed Salah kunasa.
Lakini baada ya mambo kwenda sawa kwa Uhamisho wa Kudumu wa Andre Schurrle kwenda Wolfsburg kwa Pauni Milioni 22 na Mohamed Salah kutua Fiorentina kwa Mkopo wa Miezi 6, Chelsea imeweza kumnunua Juan Cuadrado kwa Dau linalodaiwa kufikia Pauni Milioni 26.8.
Inaaminika Cuadrado, ambae alishapimwa Afya yake mapema Leo huko Stamford Bridge, atasaini Mkataba wa Miaka 4 na Nusu.



Yakubu arejea England
Nae Mchezaji wa Kimataifa wa Nigeria, Yakubu Aiyegbeni, amerejea England baada kusaini kuichezea Reading kama Mchezaji Huru na hiyo itakuwa Klabu yake ya 6 kuichezea Nchini humo.

Akiwa England, Yakubu, mwenye Miaka 32 na ambae Klabu yake ya mwisho ni Al Rayyan ya Qatar, ashawahi kuzichezea Klabu za Portsmouth, Middlesbrough, Everton, Leicester City na Blackburn Rovers.
Yakubu aliihama Blackburn Rovers Mei 2012 na kwenda huko China kuichezea Guangzhou FC.

Zaha arudi Crystal Palace
Crystal Palace wamemsaini tena Winga wao Wilfried Zaha kwa dili ya kudumu kutoka Manchester United.
Zaha, mwenye Miaka 22, alihamia Man United Miaka Miwili iliyopita kwa Dili ya Pauni Milioni 15 lakini alishindwa kupata Namba na Msimu huu akawa huko Palace kwa Mkopo.

Orodha ya wachezaji waliosajiliwa katika EPL katika dirisha dogo la usajili mwezi Januari, lililofungwa jana. (Bei kwa pauni za Kiingereza kwenye mabano - Undisclosed- kiwango ambacho hakijatajwa, Loan- mkopo)
Arsenal: Krystian Bielik (£2.4m), Gabriel Paulista (£11.2m)
Aston Villa: Carles Gil (£3.2m), Scott Sinclair (Loan)
Burnley, Michael Keane (Undisclosed)
Chelsea: Juan Cuadrado (£23.3m)
Crystal Palace: Shola Ameobi (Free), Yaya Sanogo (Loan), Pape Souare (Undisclosed), Jordon Mutch (Undisclosed), Lee Chung-yong (Undisclosed), Wilfried Zaha (Undisclosed), Keshi Anderson (Undisclosed), Andreas Breimyr (undisclosed)
Everton: Aaron Lennon (Loan)
Hull: Dame N'Doye (Undisclosed)
Leicester: Robert Huth (Loan), Andrej Kramaric (£9m), Mark Schwarzer (Free)
Liverpool: Hakuna aliyesajiliwa
Manchester City: Wilfried Bony (£28m)
Manchester United: Sadiq El Fitouri (Undisclosed), Victor Valdes (Free), Andy Kellett (Loan)
Newcastle: Hakuna aliyesajiliwa
QPR: Mauro Zarate (Loan)
Southampton: Filip Djuricic (Loan), Ryan Bertrand (Undisclosed)
Stoke: Philipp Wollscheid (Loan)
Sunderland: Jermain Defoe (Undisclosed)
Swansea: Jack Cork (Undisclosed), Matt Grimes (£1.75m), Kyle Naughton (£5m)
Tottenham: Dele Alli (Undisclosed)
West Brom: Callum McManaman (£4.75m), Darren Fletcher (Free)
West Ham: Doneil Henry (Undisclosed)

No comments:

Post a Comment