YANGA wameshindwa kuifunga Ndanda FC kwenye Mechi ya Ligi Kuu Vodacom iliyochezwa hii Leo Uwanja wa Taifa Mjini Dar es Salaam na kwisha 0-0.Matokeo haya yamewafanya Yanga wapande hadi Nafasi ya Pili wakiwa Pointi 2 nyuma ya Vinara Azam FC ambao wana Pointi 21 huku wote wakiwa wamecheza Mechi sawa 11 kila mmoja.
Nafasi ya Tatu imeshikwa na Mtibwa Sugar ambao wana Pointi 18 kwa Mechi 11.
Laiti kama Yanga wangeifunga Ndanda FC basi wangeipiku Azam FC uongozo wa Ligi hii.
Mechi inayofuata kwa Yanga ni hapo Jumatano Februari 4 huko Mkwakwani Mjini Tanga dhidi ya Coastal Union.
No comments:
Post a Comment