BUKOBA SPORTS

Sunday, February 1, 2015

ARSENAL 5 vs 0 ASTON VILLA, GUNNERS WAPANDA NAFASI YA TANO!! HECTOR BELLERIN AFUNGA BAO, OZIL, WALCOTT NA CAZORLA WAFUNGA BAO!

Theo Walcott dakika ya 63 kipindi cha pili aliipachikia Arsenal bao la tatu na kufanya 3-0. Dakika ya 75 Santi Cazorla aliiongezea bao tena la nne Arsenal kwa mkwaju wa penati na kufanya 4-0, Mchezo uliopigiwa kwenye Uwanja wa Emirates na kushuhudiwa na Mashabiki 59,958. Bao la 5 lilifungwa na Hector Bellerin dakika za lala salama za nyongeza na kufanya 5-0 dhidi ya Aston Villa. Ushindi huu wa 5-0 Umempandisha  Arsenal nafasi ya tano kwa kuishusha Spurs akiwa na pointi 42 sawa Southampton ambao wanakipinga punde na timu ya Swansea City baada ya muda mfupi. Kwa Aston Villa wameshuka hadi nafasi ya 16 na pointi zao 22.Mesut Özil akishangilia bao lake.Mesut Özil aliipa bao la pili Arsenal kipindi cha pili dakika ya 56 na kufanya 2-0Olivier Giroud Aliipatia bao la kwanza Arsenal dakika ya 8 kipindi cha kwanza.View image on TwitterVIKOSI:
Arsenal wanaoanza: Ospina, Bellerin, Mertesacker, Koscielny, Monreal, Coquelin, Ramsey, Walcott, Cazorla, Ozil, Giroud
AKIBA: Szczesny, Gibbs, Gabriel, Rosicky, Flamini, Chambers, Akpom
Aston Villa wanaoanza: Guzan, Hutton, Okore, Clark, Richardson, Delph,Gil, Sanchez, Cleverley, Benteke, Weimann
AKIBA: Sinclair, Baker, Bacuna, Agbonlahor, Westwood, Cissokho, Given 

No comments:

Post a Comment